Tshishimbi asaini miaka miwili Jangwani
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, hatimaye imemalizana na kiungo mkabaji Papy Tshishimbi Kabamba raia wa DRC kwa kandarasi ya miaka miwili, kwa maana hiyo kiungo huyo atakipiga Jangwani hadi mwaka 2019.
Papy Tshishimbi alianza kuingia kwenye rada za Yanga tangu alipokuja nchini na kikosi cha Mbabane Swallors cha Swaziland kilipocheza na Azam FC mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga ilikuwa ikihaha kutafuta kiungo mkabaji namba sita kwa muda mrefu baada ya kuondokewa na mafundi Athuman Iddi 'Chuji' na Frank Domayo ambao waliweza kumudu kucheza nafasi hiyo, Tshishimbi alifuzu vipimo vya afya na kuingia rasmi mkataba leo mchana