Mtibwa Sugar yalamba dume kwa Dilunga
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Timu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake katika mashamba ya miwa yaliyopo Turiani, mkoani Morogoro leo imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo fundi Hassan Dilunga.
Dilunga mmoja kati ya viungo bora kabisa hapa nchini aliyewahi kuichezea Yanga SC kwa mafanikio lakini ameangukia kwa Wakata miwa hao.
Dilunga anaungana na straika chipukizi wa Ndanda FC, Riffat Khamis ambaye naye amesaini kujiunga na timu hiyo, mbali na nyota hao, tayari Mtibwa Sugar imeshafanikiwa kumnasa Salum Kanoni ambaye aliwahi kucheza Simba