GOR MAHIA YAITAKA SIMBA,SIMBA DAY

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Dylan Kerr amesema angependa kama klabu yake ya zamani ya Simba SC itawaalika kuja kucheza nao katika tamasha la Simba Day hapo Agosti 8 mwaka huu.

Kerr aliyasema hayo hivi karibuni wakati timu yake ya Gor Mahia ilipokuwa hapa nchini ambapo pia ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Everton ya Uingereza.

Kocha huyo amewahi kuifundisha Simba SC lakini baadaye akaondolewa kwenye kikosi hicho hasa baada ya timu kufanya vibaya, hata hivyo Kerr amedai angefurahi kama Simba itacheza na Gor Mahia ili awaonyeshe kitu na wajutie kumuacha

Dylan Kerr, kocha wa Gor Mahia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA