Mtibwa Sugar yamrejesha Kado
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam.
Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kumrejesha mlinda mlango wake wa zamani, Shaaban Kado ambaye alikuwa anaichezea Mwadui FC ya Shinyanga.
Kocha wa timu hiyo Zuberi Katwila amesema baada ya kuondokewa na kipa wao chaguo la kwanza, Said Mohamed Nduda ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, alimpendekeza Kado.
Uongozi wa Mtibwa Sugar umeona ni bora umrejeshe Kado ambaye alikuwepo hapo kabla hajaenda kujiunga na Yanga SC, Kado ameamua kurejea kwani hadi sasa Mtibwa imemnyakua mlinzi wa Mwadui, Salum Kanoni, Kado amesaini mkataba wa miaka miwili