MAMBO UWANJANI WAANZISHA TV YAO
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Tovuti inayokuja juu kwa sasa hapa nchini hasa kwa utayarishaji na uandishi wao mzuri wa habari wa Mambo Uwanjani Blogspot wenye makazi yake jijini Dar es Salaam umefungua Tv yake ya Online.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani, Prince Hoza amesema, ni kweli Mambo Uwanjani wameanzisha tv yao inayopatikana kupitia chanel ya youtube.
Hoza amesema tv yao inaitwa Mambo Spoti Tv ama kwakifu MSTV ambapo amewataka wapenzi wa Mambo Uwanjani kutembelea tv yao kupitia youtube na amedai wataanza pia kurusha mpira live.
"MSTV ipo kwa ajili ya michezo, burudani na vichekesho, na wala hatutadili na siasa wala mambo mengine yasiyotuhusu", alisema Hoza ambaye pia ni mwandishi wa makala za uchambuzi katika gazeti la Msimbazi