Azam FC yabutwa na Mji Njombe
Na Mwandishi Wetu. Njombe
Timu ya Mji Njombe jioni ya leo imefanikiwa kuwasambaratisha mabingwa wa Afrika mashariki na kati, Azam FC ya jijini Dar es Salaam mabao 2-0 mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Mji Njombe.
Ikicheza kwa kutumia karibu nyota wake wote wakiwemo wale wa kimataifa, vijana wa Mji Njombe ambao msimu ujao watacheza Ligi Kuu bara walifanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika ya 34 kipindi cha kwanza lililofungwa na Adam Baiko.
Hadi mapumziko Mji Njombe walikuwa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Azam walikuja na nguvu mpya baada ya kuwatoa wachezaji wake 11 na kuingiza wengine lakini hawakumzuia Raphael Siame ambaye alifunga bao la pili dakika ya 80.
Huo ni mchezo wa pili kwa Azam tangu waanze ziara yao ya Nyanda za juu kusini, katika mchezo wa kwanza, Azam ilitoka suluhu na Mbeya City