HUMUD,TEGETE WAENDA MAJIMAJI
Na Mwandishi Wetu. Ruvuma
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Jerryson Tegete na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Simba SC, Abdulhalim Humud wote kwa pamoja wamejiunga na Majimaji ya Songea kwa ajili ya msimu ujao.
Majimaji inayonolewa na Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Kajumulo World Soccer , Kalimangonga Mtoro Ongala wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.
Tegete ambaye alikuwa akiichezea Mwadui FC ya Shinyanga ameamua kubadili upepo na kujiunga na timu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mara mbili, Humud naye alikuwa akicheza soka la kulipwa nchini Oman