Safari ya Msuva Morocco imeiva

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam.

Baada ya jana kuwaaga Wanayanga, kiungo Simon Msuva anatarajia kuondoka nchini kuelekea Morocco kujiunga na klabu ya Difaa El Jajida inayoshiriki Ligi Kuu.

Awali Msuva ilikuwa akajiunge na klabu moja ya nchini Afrika Kusini, lakini Waarabu hao wa Morocco wamemfuata hadi Afrika Kusini alikokuwa na timu ya taifa iliyokuwa inashiriki michuano ya Cosafa Castle Cup.

Hata hivyo Msuva anayekwenda kujiunga na timu hiyo ambayo tayari imemnasa Mtanzania mwingine, Ramadhan Singano "Messi" ambaye alikuwa anaichezea Azam FC, malengo yake ni kwenda kucheza Ureno au Hispania.

Msuva jana ilikuwa aambatane na timu ya taifa, Taifa Stars iliyokwenda Rwanda kurudiana nao Jumamosi ijayo lakini safari yake ikaishia Uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kutakiwa haraka na Waarabu hao hivyo sasa anashughurikia safari yake

Simon Msuva, anaondoka Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA