Msuva kimeeleweka Morocco, kesho anapaa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka hapa nchini, Simon Msuva anatarajiwa kuondoka nchini kesho kuelekea nchini Morocco tayari kabisa kujiunga na timu yake mpya ya Difaa El Jajida.
Msuva atapaa kesho jioni akiwa na uhakika kabisa wa kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo, Msuva ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, amecheza kwa mafanikio makubwa akiwa na klabu yake ya Yanga.
Difaa El Jajida imemchukua Mtanzania mwingine Ramadhan Singano "Messi" wa Azam FC, Msuva anaungana pia na nyota Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Elius Maguli na Farid Musa ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi