Ronaldo wa Ndondo Cup atua Mbeya City
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Wagonga Nyundo wa Mbeya City ya jijini Mbeya imeendelea kujiimarisha baada ya kufanikiwa kuwasainisha wachezaji wawili kwa mkupuo.
Wagonga nyundo hao jana wamekamilisha usajili wa Antony Mwingira na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Ashanti FC na KCM zote za Dar es Salaam, Iddi Seleman maarufu kama Ronaldo.
Ronaldo anasifika sana kwa uchezaji wake katika michuano ya Ndondo Cup inayochezwa jijini Dar es Salaam, kiungo huyo amekuwa akizivhezea timu mbalimbali ikiwemo Faru Jeuri, wachezaji wote hao wamesaini mkataba wa miaka miwili