Rasmi,Msuva asaini El Jajida
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Simon Happygod Msuva amesaini mkataba wa kujiunga na timu ya Ligi Kuu ya Difaa El Jajida ya Morocco lakini klabu hiyo imefanya siri haijaweka wazi mkataba huo ni wa muda gani.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo mchana wa leo imesema kwamba, Difaa El Jajida imemalizana na mchezaji huyo na tayari imeshamtambulisha kwa mashabiki wake.
Aliyekuwa katibu wa Yanga Sc, Dk Jonas Tiboroha anahusika katika usajili huo akianza kupatana na kumuuza pia, inasemekana Yanga itapatiwa Dola 150,000 ambazo ni sawa na shilingi Milioni 300 za Kitanzania.
Msuva anaungana na winga mwingine wa Tanzania, Ramadhan Singano "Messi" ambaye alikuwa anaichezea Azam FC, Msuva alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Moro United ambayo nayo ilimchukua akitokea Akademia ya Azam FC