Peter Manyika atolewa kwa mkopo
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mlinda mlango Peter Manyika Jr anatolewa kwa mkopo wakati kipa mwingine Dennis Richard ametemwa rasmi.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe amesema leo kuwa wameamua kumtoa kwa mkopo Manyika Jr kwakuwa akarejeshe kiwango.
Manyika ameonekana kushuka kiwango na ndio maana hakuwa akianza katika kikosi cha kwanza, pia Hanspoppe amesema Simba imewaacha Novat Lufunga, Hamad Juma, Pastory Athanas, Janviel Bokungu na Dennis Richard.
Mwenyekiti huyo amesifu usajili walioufanya na kudai umezingatia mahitaji ya mwalimu Joseph Omog na msaudizi wake Jackson Mayanja