Hatimaye mrithi wa Niyonzima asaini Yanga
Na Ikram Khamees. Morogoro
Hatimaye klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo fundi wa Mbeya City na timu ya taifa, Taifa Stars, Raphael Daudi ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji huyo anaungana na kikosi hicho kesho, Yanga imeweka kambi mjini hapa ikijiandaa na mchezo wake wa Ngao ya Jamii na mahasimu wao Simba mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Daudi anakuwa mchezaji wa nane kusajiliwa na Yanga akiungana na Abdallah Shaibu "Ninja" kutoka Taifa Jang' ombe ya Zanzibar, Ibrahim Ajibu kutoka Simba, Pius Buswita kutoka Mbao FC.
Wengine ni Youthe Rostand kutoka African Lyon, Ramadhan Kabwili (Huru) na Burhan Akilimali (Huru ), Daudi ni mrithi wa Niyonzima aliyekwenda Simba