Aishi Manula amgwaya Nduda Simba

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kipa chaguo la kwanza wa timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula amesema hawezi kujiunga na Simba SC kwa sasa mpaka pale mkataba wake na Azam FC utakapomalizika.

Manula amedai kwa sasa anajipanga kurejea Azam kwani anaheshimu mkataba wake ambao utamalizika katikati ya Agosti mwaka huu, ameongeza kuwa anataka kuwasiliana ma meneja wa Azam, Philipo Arando ili ampe maelekezo na aingia kambini.

Azam imefanya ziara katika mikoa ya nyanda za juu Kusini hivyo na yeye atalazimika kuwafuata, hii ina maana kwamba hatojiunga na Simba kama inavyoelezwa kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili.

Lakini taarifa za chini kwa chini zinasema kipa huyo amemkacha kipa mwenzake Said Mohamed Nduda ambaye naye amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, Nduda naye ni kipa wa timu ya taifa, Taifa Stars na alipangwa mara moja katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Lesotho ambapo alidaka vizuri na kuchaguliwa kipa bora wa mashindano ya Cosafa Castle Cup yaliyofanyika Afrika Kusini Julai mwaka huu

Aishi Manula anarejea Azam FC

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA