Kambi ya Simba, South usipime
Na Exipedito Mataruma. Afrika Kusini
Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC wamepiga kambi hapa Afrika Kusini wakifanya mazoezi yao katika Uwanja wa Edenvale uliopo hapa Afrika Kusini, timu hiyo inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog na msaidizi wake Jackson Mayanja inafanya mazoezi ya hatari.
Simba iko hapa ikijiandaa na mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga SC mchezo utafanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba imekuja hapa na wachezaji 12 na nyota wake wengine waliokuwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars nao watajiunga na wenzao hivi punde hasa baada ya jana kuondoshwa katika michuano ya Chan, Ingia Youtube tumewawekea video ya mazoezi ya Simba