STRAIKA LA MABAO LA GHANA HILI HAPA MSIMBAZI
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Simba SC sasa imepania kwenye suala la usajili kwani imeamua kusajili wachezaji wote nyota ndani ya nje ya Tanzania, Nicholaus Gyan raia wa Ghana ndiye straika mpya anayetarajia kutua katika klabu hiyo.
Gyan ameonyesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu ya Ghana huku akifanikiwq kufunga mabao 12, straika huyo unaambiwa ni hatari kinoma na Wekundu wa Msimbazi wamepanga kumshusha hivi karibuni.
Hadi sasa Simba imeshasajili wachezaji 12 na inadaiwa kuna wengine wawili watasajiliwa, Gyan ameshawekwa katika orodha ya watakaosajiliwa na kitu kinachosubiriwa kwa sasa ni ujio wake tu, Gyan atasimama namba tisa na anasifika kwa mashuti