Tizi la Yanga Morogoro kama Ulaya
Na Ikram Khamees. Morogoro
Asikwambie mtu, Yanga SC wanapiga zoezi la hatari kama vile vilabu vya Ulaya, Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Mzambia George Lwandamina anaendelea kukiweka fiti kikosi cha Yanga ambacho Agosti 23 kitavaana na mahasimu wao Simba SC.
Mzambia huyo amekuwa akiwapa mazoezi mbalimbali ambayo pia yamekuwa yakifanywa na vilabu vikubwa barani Ulaya kama FC Barcelona, Real Madrid, Chelsea, Manchester United, Manchester City, Liverpool, Arsenal, Ac Milan na nyinginezo.
Baadhi ya mashabiki wanaojitokeza kushuhudia mazoezi hayo wanasema kama kikosi hicho kitafungwa katika mechi zake zijazo basi hakina bahati kwani zoezi wanaloliona ni hatari, shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mau amedai Yanga itatetea ubingwa wake.
Baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa kivutio ni pamoja na Mzambia Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu, Juma Abdul na kiberenge Baruhan Akilimali, Yanga itacheza mchezo wa kirafiki na Singida United