Rooney apiga bonge la bao, Samatta achomoa
Mshambuliaji Wayne Rooney jana alifunga bonge la goli katika mchezo wa kirafiki baina ya Everton ya Uingereza na KRC Genk ya Ubelgiji ulioisha kwa sare ya bao 1-1.
Mtanzania Mbwana Samatta aliisawazishia Genk katika dakika ya 55 na kufanya matokeo yawe sare sare maua, Everton wapo katika maandalizi ya msimu ujao na juma lililopita ilikuwa katika ardhi ya Tanzania ambapo ilicheza na Gor Mahia ya Kenya na kushinda mabao 2-1.
Wayne Rooney amekuwa katika mwanzo mzuri tangu ajiunge na timu hiyo akitokea kwa Mashetani Wekundu, Manchester United, staa huyo amekuwa akifunga karibu mechi zote ilizocheza Everton