Wallace Karia aweka wazi uraia wake
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kaimu Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) Wallace Karia leo ameweka wazi uraia wake baada ya kuwekewa pingamizi na Iman Madega.
Karia ambaye pia ni makamu wa Rais wa Shirikisho hilo na mgombea nafasi ya Urais, aliwekewa pingamizi na mgombea mwenzake Iman Madega kuwa siyo raia wa Tanzania kama sheria inasema.
Karia amedai yeye ni Mtanzania wa kuzaliwa lakini ana asili ya Somalia, akizungumzia hilo, Karia ameshangazwa na mgombea mwenzake aliyemwekea pingamizi akidai ni wivu tu kwake.
Ameongeza kuwa wapo Watanzania kadhaa ambao wameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi lakini ni Waarabu au Wahindi ingawa ni raia wa Tanzania kama ilivyo kwake yeye