YANGA NA RAPHAEL DAUDI WAFIKA PATAMU
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, wamefikia pazuri na kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi ambapo sasa anaweza kumwaga wino kwa ajili ya kujiunga nao hiyo kesho.
Yanga walianza kumwania Daudi tangu mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara, lakini mipango haikuweza kukamilika, mabingwa hao waliingia tena kutaka saini yake baada ya kuondokewa na kiungo wake wa kimataifa, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda anayedaiwa kujiunga na Simba.
Uongozi wa Mbeya City leo umethitisha kumruhusu kiungo huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa, Taifa Stars akakipigeJangwani, naye mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga , Hussein Nyika amesema wao na Daudi watamalizana hivi karibuni lakini duru zinasema kesho mchana