Tenga aula CAF
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Rais wa zamani wa Shirikisho la kandanda hapa nchini, (TFF), Leodegar Chila Tenga amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa kamati ya ufundi na maendeleo wa Shirikisho la kandanda barani Afrika, (CAF).
Tenga ambaye ni mjumbe wa heahima wa TFF amepata nafasi hiyo kupitia mkutano wa CAF uliofanyika Rabat, Morocco ambao pia ulipitisha maazimio mbalimbali.
Naye Kaimu Rais wa TFF, Walace John Karia amemtumia salamu za pongezi Tenga na kusema hiyo ni nafasi adimu kwa Tanzania, Karia amesema kitendo na Tenga kuteuliwa kuwa makamu wa Rais wa kamati hiyo ya ufundi na maendeleo kunadhihiriaha Tanzania kulivyojaaliwa viongozi wa soka