NDEMLA NAYE KUTIMKIA SWEDEN

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kiungo mwenye mashuti wa Simba SC, Said Khamis Ndemla naye anatarajiwa kuelekea nchini Sweden tayari kabisa kujiunga na timu ya Ligi Kuu, AFC Eskilistuna ambayo pia anaichezea Mtanzania Thomas Ulimwengu.

Eskilistuna ilimuhitaji Ndemla tangia mwishoni mwa msimu uliopita lakini Simba SC ikakataa kumuachia akajiunge na timu hiyo kwa madai bado wanamuhitaji, lakini sasa endiketa ya kijani imewaka.

Simba ambayo imemnasa Haruna Niyonzima kutoka Yanga ina kila sababu ya kumruhusu Ndemla akajaribu bahati yake, inasemekana kiungo huyo ataondoka baada ya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Simba, Agosti 23 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Said Ndemla (Kushoto) anaelekea Sweden kucheza soka la kulipwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA