Kisa Malinzi, Zanzibar yaporwa uanachama Caf
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Shirikisho la kandanda Barani Afrika, (CAF) limeipoka uanachama Zanzibar na bado haijafahamika kipi kilichopelekea Shirikisho hilo kuipoka uanachama.
Taarifa za Zanzibar kuporwa uanachama wake zimewashangaza wengi lakini chanzo kimoja cha habari kinasema Rais wa Shirikisho la kandanda nchini, (TFF) Jamal Malinzi amehusika.
Inasemekana Caf imeipoka uanachama Caf ambayo majuzi tu ikiwapa uanachama kamili ambao ungeifanya timu ya taifa ya Zanzibar kuweza kushiriki michuano ya mataifa barani Afrika, lakini sasa haitaweza kushiriki tena.
Inasemekana rais mpya wa Caf na kamati yake wameona ni bora kuipoka uanachama Zanzibar kwavile Jamal Malinzi alikuwa akimuunga mkono Issa Hayatou