Azam FC yaibutua Lipuli ya Seleman Matola 'Veron'
Na Mwandishi Wetu. Iringa
Timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam imefufua matumaini baada ya kuilaza Lipuli ya Iringa mabao 4-0 mchezo wa kirafiki uliopigwa leo. Azam ilianza vibaya ziara yake ya nyanda za juu kusini baada ya kupoteza mechi zake mbili moja ikitoka sare tasa na Mbeya City 0-0 na nyingine kufungwa na Mji Njombe 2-0.
Kikosi cha Azam kinachonolewa na Mromania, Aristica Cioaba kilianza kuonyesha kandanda safi tofauti na ilivyocheza na Mji Njombe na kuweza kujipatia ushindi huo mkubwa siku ya leo, Lipuli iliyopanda daraja ikiwa chini ya kocha Seleman Matola 'Veron' ambaye amewahi kuichezea Simba SC na baadaye kuwa kocha msaidizi imeweza kuwasononesha mashabiki wake.
Mabao ya Azam FC yalifungwa na Yakubu Mohamed, Waziri Junior, Yahya Zayid na Salum Abubakar "Sure Boy", Azam imeweka kambi nyanda za juu kusini ikijiandaa na Ligi Kuu Bara