Mdogo wake Yahaya Akilimali asaini Yanga
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, jana imemsainisha kiungo mshambuliaji Baruan Akilimali ambaye ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Yahaya Akilimali.
Kiungo huyo ilikuwa atue Lipuli ya Iringa, lakini mabingwa hao wa Bara wamemua kumpa mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo ambayo tayari imeshaondokewa na winga wake Simon Msuva.
Akilimali anatajwa mmoja kati ya mawinga wenye mbio ambapo mashabiki wa soka wamempachika jina la Kiberenge ambacho kinasemekana kinakimbia kuliko gari