Rage aichambua Zanzibar, asema haikustahili kupewa uanachama Caf
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ameichambua Zanzibar na kudai haikustahili hata kidogo kupewa uanachama hata wa muda na Shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika, (CAF) na waliojaribu kuipa walikosea sana.
Akizungumza jana, Rage amesema Zanzibar haina hadhi ya kupewa uanachama na CAF kwakuwa siyo nchi kamili inayotambuliwa na Umoja wa mataifa na Afrika pia.
Amefafanua kuwa nchi inayotambulika na kupewa uanachama ni ile mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), amezitaja nchi zilizopata uanachama ambazo si nchi kamili kama Zanzibar kuwa ni Ireland, Scotland, Trinidad and Tobacco na Wiles kuwa hizo zilipewa kwakuwa Uingereza ndiyo mwanzilishi wa FIFA.
Rage amedai Zanzibar ni sehemu ya Tanzania hivyo nchi moja haiwezi kuwa na wanachama wawili na amewataka Wazanzibar kwa hili wawe wapole