Singida United wafunga usajili kwa Kigi Makasi
Na Paskal Beatus. Mwanza
Timu ya Singida United imefanikiwa kukamilisha usajili wake baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ndanda FC, Kigi Makasi kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa uongozi wa Singida United umesema kuwa Kigi anakuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa na timu hiyo baada ya kumaliza kwa wachezaji wa kimataifa.
Timu hiyo kwa sasa itakuwa imeshawasajili wachezaji 15 huku wachezaji saba pekee wakiwa wa kimataifa kutoka nchi za Zimbabwe, Rwanda na Uganda, Hans Van der Pluijm ndiye kocha mkuu wa kikosi hicho kilichopanda Ligi Kuu