Akina Malinzi kuendelea kusota
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) Jamal Malinzi na wenzake, katibu wa TFF, Celestine Mwesigwa na mkurugenzi wa fedha wa Shirikisho hilo, Isiande Isowafe imepigwa kalenda.
Kesi hiyo imesogezwa hadi Agosti 11 mwaka huu, Malinzi na wenzake walifika mahakamani Kisutu leo na hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri lao akaamua kuipiga kalenda kesi hiyo hivyo Malinzi na wenzake wamerudishwa tena rumande hadi Agosti 11.
Kusogezwa mbele kwa kesi hiyo kunapisha upepelezi ambapo ukikamilika basi viongozi hao wanaweza kuhukumiwa, na kama ushahidi kamili utakosekana basi wanaweza kuachiwa, tayari Malinzi ameshaachia ngazi nafasi ya Urais na sasa Walace Karia anakaimu nafasi yake