Chuji Busungu, Seme nao kimeeleweka

Kiungo wa zamani wa Yanga na Simba Athuman Idd 'Chuji' amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu ya Ligi Kuu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara.

Chuji aliwahi kutamba kwenye vilabu vya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti zote akizichezea mara mbili mbili, lakini alijiunga na Mwadui ya Shinyanga ambayo nayo aliachana nayo kabla ya msimu uliopita kujiunga na timu ya daraja la kwanza ya KCM ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Naye mshambuliaji wa zamani wa Mgambo JKT na Yanga, Malimi Busungu amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Lipuli ya mjini Iringa ambayo nayo itashiriki Ligi Kuu Bara.

Wakati Busungu akisaini kujiunga na Lipuli, kiungo mwingine wa zamani wa Yanga na Ndanda, Omega Seme amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Lipuli

Omega Seme, mwenye jezi nyekundu, akitambulishwa kujiunga na Lipuli
Malimi Busungu (Katikati) akitambulishwa kutua Lipuli
Athuman Idd "Chuji" akisaini Ndanda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA