Milioni 300 zamng' oa Msuva Yanga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Klabu ya Difaa El Hassan Jajida ya Morocco itailipa Yanga SC karibu Dola 150,000 ambazo ni sawa na shilingi Milioni 300 za Kitanzania ili kumnyakua kiungo mshambuliaji mwenye kasi ya ajabu, Simon Msuva.
Mipango ya kumng'oa Msuva ilianza tangu kumalizika kwa msimu uliopita na jamaa walianza kumfukuzia hadi timu ya taifa ilipokuwa Afrika Kusini kushiriki michuano ya kombe la Cosafa Castle Cup.
Msuva jana alishindwa kuondoka na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ambapo ilielekea nchini Rwanda kwa ajili ya kurudiana na timu ya taifa ya nchi hiyo mchezo wa mataifa ya Afrika maarufu Chan na alikuwa akiangaikia taratibu za kusafiri.
Kwa maana hiyo Msuva anaungana na Mtanzania mwenzake Ramadhan Singano "Messi" ambaye tayari ameshajiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu, kwa sasa kinachongojewa kwa Msuva ni kipimo cha afya yake