Kaseke naye atua Singida United

Na Paskal Beatus. Dar es Salaam

Timu ya Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Mholanzi, Hans Van der Pluijm, jana imekamilisha kandarasi ya winga wa Yanga, Deus Kaseke kwa kipindi cha miaka miwili.

Kaseke amekubali kutua kwenye timu hiyo iliyojaza nyota lukuki wa Afrika mashariki, Kaseke anakuwa mchezaji wa nne kuondoka katika kikosi cha Yanga ndani ya wiki moja baada ya Simon Msuva aliyetua Difaa Hassan El Jajida, Deo Munishi "Dida" aliyekwenda Afrika Kusini na Ally Mustapha 'Barthez' aliyejiunga na Singida United.

Kuondoka kwa Kaseke ndani ya Yanga kunaleta wasiwasi mkubwa kwenye kikosi hicho kwani mchezaji huyo aliisaidia Yanga kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo, akiwa kwenye ubora wake Kaseke aliiwezesha pia Mbeya City kutikisa soka la Tanzania

Deus Kaseke (Kulia) akitambulishwa kujiunga na Singida United

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA