Tanzania yatupwa nje CHAN

Na David Pasko. Rwanda

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imetupwa nje ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN) baada ya kulazimishwa sare tasa 0-0 na wenyeji Rwanda (Amavubi) katika mchezo wa marudiano uliofanyika Uwanja wa Nyamirambo, mjini Kigali.

Wenyeji Rwanda walikuwa wanahitaji sare tasa ama ushindi wa aina yoyote kwakuwa tayari wana bao moja la ugenini walilolipata jijini Mwanza baada ya kulazimisha sare ya mabao 1-1 na Taifa Stars.

Kocha wa Tanzania Salum Mayanga leo amewaanzisha Simon Msuva, Muzamil Yasini, John Bocco 'Adebayor na Shiza Kichuya lakini hawakuweza kupenya ukuta wa Rwanda ambao sasa wanakwenda kukutana na Uganda katika mchezo ujao.

Kwa maana hiyo Taifa Stars imeondoshwa kwenye michuano hiyo nanitaendelea kuwa mtazamaji, wachezaji wa kikosi hicho sasa watarejea kwenye vilabu vyao kwa ajili ya nashindano yajayo

Kikosi cha Stars kimetolewa 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA