BABU MWANJALE NAHODHA MPYA SIMBA
Na Mwandishi Wetu. Afrika Kusini.
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo imemvua rasmi unahodha Jonas Mkude na kumpachika Mzimbabwe Method Mwanjale "Babu" ambaye atasaidiwa na John Bocco "Adebayor" na Mohamed Hussein "Tshabalala".
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara imesema kuwa Mwanjale atakuwa nahodha mpya wa klabu hiyo badala ya Jonas Mkude ambaye sasa atakuwa mchezaji wa kawaida.
Haijajulikana sababu gani iliyopelekea kumuondoa Mkude katika nafasi hiyo, ingawa Mambo Uwanjani inafahamu kila kitu kuondoshwa kwa Mkude katika nafasi hiyo, Mwanjale ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu na pia ni mkongwe na ndiyo imepelekea akabidhiwe nafasi hiyo