Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2024

Huyu ndio mzee Ally Pazi Samatta

Picha
Huyu anaitwa Ally Pazi Samatta Baba yake Mbwana Samatta Huyu Mzee alizaliwa 1943 Mkoani Pwani. Enzi yake alikuwa mwajiliwa wa jeshi la Polisi Mzee Samatta alicheza sehemu ya ushambuliaji namba 10. Timu alizochezea timu ya Polisi Moro 1962- 1963 Canada Dry 1963-1964 Simba (Sunderland) 1964-1965 Cosmopolitan 1968-1969. Pia alichezea timu ya Taifa, Taifa Stars na ile ya bara

Baba yake Samatta awalilia Msuva na mwanae Taifa Stars

Picha
"Inaonekana kuna aina fulani ya chuki kutokana na mafanikio ya mwanangu Mbwana, bado Mbwana ana nafasi kubwa sana katika timu ya taifa, Samatta na Msuva ni wachezaji muhimu sana kwenye taifa letu, kwa asilimia kubwa wao ndio wamesababisha tufuzu kucheza AFCON zote mbili "Kwenye kombe la dunia 1966, Pele alipata majeraha dhidi ya Ureno lakini mechi iliyofuata alicheza kwa sababu alipigwa sindano ya ganzi na wakawa wanamuogopa sababu yupo nje; hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa Samatta vivyo hivyo kwa Msuva Kocha Hemed Morocco amekosea sana kuwaacha Samatta na Simon Msuva, Mzee Ally Samatta Baba mzazi wa Mbwana Samatta

Simba, Al Hilal hakuna mbabe

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika uwanja wa KMC Complex Kinondoni jijini Dar es Salaam. Simba walitangulia kupata kupitia kwa mshambuliaji mpya aliyetambulishwa kwenye mchezo huo Lionel Atebe dakika ya 26, kabla ya Al Hilal inayonolewa na Ibenge raia ya DR Congo dakika ya 76 kupitia kwa Serge Pokou. Hata hivyo Suleiman Ezala wa Al Hilal dakika ya 55 alioneshwa kadi nyekundu na kushindwa kuendelea na mchezo, Simba itaendelea kushuka tena ueanjani kucheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa 

Pyramids mabingwa wa Misri, Mayele ahusika

Picha
Mshambuliaji Fiston Mayele raia wa DR Congo, amekuwa na msimu mzuri baada ya kuisaidia timu yake ya Pyramids ya Misri kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Mayele amrhusika kwa asilimia 100 timu hiyo kushinda ubingwa huu kwani yeye ndiye chachu kubwa ya timu kuhahakisha inapata ushindi wastani kwa kila mechi. Mshambuliaji huyo aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga SC ya Tanzania ambayo nayo aliipa ubingwa misimu miwili mfululizo, mpaka msimu unamalizika, Mayele aliibuka mfungaji bora wa klabu hiyo. Mayele amefunga magoli 17 ambapo pia ameweza kuwa mfungaji bora namba mbili wa ligi ya nchi hiyo

Azam FC yafurusha benchi lote la ufundi

Picha
Klabu ya Azam FC  imeachana na benchi lake lote la Ufundi likiongozwa na Kocha Yousouph Dabo  Taratibu zote za uvunjwaji wa mikataba umeshamalizika na benchi la Ufundi limeshalipea stahiki zao

Godbless Lema aziombea mabaya Simba na Yanga

Picha
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Godbless Lema amewashangaa Watanzania kuendelea na msingi wa mawazo kwamba Simba na Yanga zina maana sana kuliko kujali maisha ya watu. Lema amedai kwamba kama angekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu ili aziue kabisa timu hizo kwani zinachelewesha maisha ya Watanzania. Mwanasiass huyo aliyerejea nchini baada ya kuwa uhamishoni wakati wa utawala wa Awamu ya tano chini ya Dkt John Magufuli, anadai maisha ya Watanzania yanahitaji fikra pana, lakini Simba na Yanga zinaharibu mipango kwani kila mtu anawaza Simba na Yanga. "Watanzania mkiendelea na huu msingi wa mawazo mliyonayo ya kwamba Mpira wa Simba na Yanga unamaana kuliko maisha ya wenzenu, hii nchi ni ya ajabu. Mimi ningekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu aziue SIMBA na YANGA zisiwepo nchi hii ningeshukuru sana'' Alisema Godbless Lema

Wydad Casablanca bado inahaha kumnasa Mzize

Picha
Wydad Casablanca hapo jana imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu Nchini Morocco Maarufu kama Botola Pro. Wydad iliyosheheni wachezaji wapya na Benchi la ufundi jipya bado wanakazi ya kufanya kuhakikisha wanarejea katika ubora wao wakawaida. Baada ya kupoteza mchezo huo mashabiki wa Wydad Casablanca wameishinikiza klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa kimataifa kutoka Tanzania Clement Mzize. Bado nafasi ipo ya kumsajili kwani dirisha la usajili linafungwa September 19 2024.

CEO Bodi ya Ligi asema VAR rasmi kutumika Ligi Kuu

Picha
CEO wa Bodi ya Ligi kuu (TPBL) Almas Kasongo amesema VAR imeshafika Tanzania na imetolewa na CAF na tayari waamuzi wameshaanza mafunzo maalum ya kutumia kwenye michezo ya NBC Premier League na mafunzo yakishakamilika watapata kibali cha matumizi yake kutoka FIFA na CAF. .

MVP wa Simba aumia ghafla, kuikosa Al Hilal kesho

Picha
Taarifa za kuaminika ni kuwa kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua atakosekana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Al Hilal ya Sudan. Jean Charles Ahoua atakosekana katika mchezo huo kwasababu ya majeraha ambayo ameyapata. Wakati huo huo kiungo mwingine wa Simba, Mkongoman Fabrice Ngoma ataukosa mchezo huo baada ya kuondoka kikosini kuelekea nyumbani kwao DR Congo ambapo ana matatizo ya kifamilia

Ateba kutesti mitambo na Al Hilal Omdurman

Picha
Mshambuliaji mpya wa Club ya Simba SC raia wa Cameroon Leonel Ateba Mbida atatumia jezi namba 13 akiwa Simba SC. Atacheza kwa mara ya kwanza akiwa katika jezi ya Mnyama kesho Jumamosi dhidi ya Al Hilal Omdurman katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki

Haji Mnoga akamilisha usajili Salford City

Picha
Beki wa kimataifa wa Tanzania, Haji Mnoga amekamilisha usajili wake kuelekea katika Klabu ya Salford City, iliyopo Jiji la Manchester Nchini Uingereza. Mnoga amesaini mkataba wa mwaka mmoja (mpaka 2025) na Klabu hiyo akitokea katika Klabu ya Portsmouth kama mchezaji huru. Salford City ni Klabu inayoshiriki Ligi daraja la pili Kiwango cha nne kwenye wa mfumo wa Ligi Nchini Uingereza. Hivi sasa iko katika nafasi ya 20 kwenye msimamo wa Ligi hiyo yenye timu 24 katika michezo mitatu.

#TupoNaMama. Barabara za kiwango cha lami zajengwa mkoa Pwani

Picha
Mtandao wa barabara za lami nchi nzima unazipi kupanuka na sasa mkoa Pwani unaendelea kujengwa, ambapo barabara za lami za kiwango cha juu zinazidi kujengwa. Jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan zimezidi kuchukua nafasi. Mkoa Pwani ulikabiliwa na uchakavu wa barabara zake ambazo nyingi hazikuwekwa lami, lakini mhe Samia amejibu maombi yao na sasa barabara za kiwango cha lami zinajengwa kila kijiji cha mkoa huo. Hongera sana mhe Rais Samia umejibu maombi ya Pwani

CEO Namungo aamua kujiuzuru

Picha
CEO wa Namungo FC, Omar Kaya amejiuzulu nafasi yake ndani ya Namungo FC kwa kuandikia barua baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi. Kaaya smbaye pia aliwahi kuwa katibu wa klabu ya Yanga SC, aliamua kujiuzuru baada ya Namungo kufanya vibaya mfululizo. "Mimi Omar Kaya leo (Jana) Agosti 30, 2024 nimewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi ya utendaji mkuu wa Namungo FC."- Omar Kaya

Azam FC kumpiga bei Feitoto msimu ujao

Picha
Baada ya kiungo mshambuliaji Feisal Salum (26) kukataa kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili katika klabu ya Azam Azam wamepanga kumuweka sokoni kiungo huyo katika dirisha kubwa lijalo la uhamisho Ofa zitakazopewa kipaumbele zaidi ni kutoka nje, ingawa Fei mwenyewe anataka kucheza Simba timu ambayo ipo moyoni mwake licha kwamba alichezea Yanga

Staa wa bongomuvi anunua gari la kifahari

Picha
Staa wa msanii wa vichekesho vya mtandaoni  Clam Cris amenunua gari kali la kifahari ambalo litamfanya awe miongoni  mwa mastaa Tanzania wanaotesa na magari mazuri na ya kuvutia. Msanii huyo ambaye kwasasa unaweza kusema ndio nambari moja akimzidi mbali Mkojani, amenunua gari kali aina ya Range Rover ni baada tu ya kurejea nchini akitokea DR Congo

Diamond, Alikiba na Harmonize kuwania tuzo za mwanamuziki bora Tanzania

Picha
Kamati ya Tanzania Music Award (TMA) leo August 29,2024 imeanza kutangaza Nominees wanaowania tuzo za muziki Nchini kwa kuanza na category tatu ambazo ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi. Wimbo bora wa taarabu wa mwaka kuna Watu na Viatu ya Malkia Layla Rashid, Hatuachani ya Amina Kidevu, Bila Yeye Sijiwezi ya Mwinyi Mkuu, Sina Wema ya Mwasiti Mbwana na DSM Sweetheart ya Salha. Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna People ya Libianca, American Love ya Qing Madi, Lonely at the Top ya Asake, Unavailable ya Davido ft Musa Keys na Mnike ya Tyler ICU. Kwa upande wa Mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume kuna Marioo kupitia wimbo wa Shisha , Diamond Platnumz kupitia Shuu, Harmonize kupitia Single Again , Alikiba kupitia Sumu na Jay Melody kupitia wimbo wa Nitasema Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema category nyingine zitaendelea ...

Yanga yaiduwaza Kagera Sugar nyumbani kwao

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga SC imeilaza Kagera Sugar mabao 2-0 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera. Huo ndio wa kwanza kwa Yangs hivyo wamefikisha pointi tatu wakati Kagera Sugar wamecheza mechi ya pili huku zote wakifungwa. Maxi Nzengeli dakika ya 26 alitangulia kufunga bao la kuongoza kwa mabingwa hao kabla ya Clement Mzize dakika ya 88 kufunga bao la pili na kuhitimisha ushindi wa mabao mawili. Wakati huo KMC FC ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex, Kinondoni, Ibrahim Elas alianza kufunga kwa upande wa KMC kabla ya Maabad Maulid kusawazisha kwa mkwaju wa penalti

Simba Queens yaangukia nafasi ya nne CECAFA

Picha
Timu ya Simba Queens imeambulia nafasi ya nne katika mashindano ya CECAFA Winners Cup kwa wanawake baada ya kufungwa mabao 2-0 na timu ya Kawempe Muslim. Mabingwa hao wa ligi ya wanawake Tanzania, imeshundwa kushangaza kwa kutupwa mapema kwenye michuano hiyo ambapo bingwa wake anakwenda kushiriki Ligi ya mabingwa Afrika. Msimu juzi Simba Queens ilienda kushiriki michuano hiyo ya Afrika na ilifika hadi nafasi ya nne, kushindwa kwa mwaka huu kumezua sintofahamu nyingi kwa wapenzi wa soka la wanawake na isitoshe timu imeandaliwa vizuri

JKT Tanzania haiwezi kugambania ubingwa na Yanga au Simba- Jemedari

Picha
Na Salum Fikiri Jr CEO wa JKT Tanzania, Jemedari Said Kazumali amedai kwamba timu yake haitaweza kugombania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara wala kufika tatu bora, isipokuwa nafasi ambayo wanaweza kushindana nayo ni ya kutoshuka daraja. Jemedari ambaye pia ni mchambuzi wa kwenye redio Crown FM inayomilikiwa na mwanamuziki Alikiba, ameshangaa kauli ikitolewa na Afisa Habari wa klabu ya JKT Tanzania Masau Bwire kwamba msimu huu wanataka kugombania ubingwa na Yanga pamoja na Simba. Jemedari amedai kwamba kushindania ubingwa na Yanga au Simba si jambo rahisi kama watu wanavyodhani, timu yake ya JKT Tanzania nafasi ambayo wanaweza kuishindania ni ya kutoshuka daraja kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo waliangukia play off

Sijawahi kusema nimestaafu soka- Bocco

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, John Raphael Bocco ameshangazwa na taarifa kwamba yeye alitangaza kustaafu soka. Bocco amesema yeye hajaacha soka na ataendelea kucheza mpaka pale atapoacha mwenyewe, Bocco alionekana akisomea ukocha na ilielezwa kwamba amestaafu soka na atakuwa kocha wa timu ya Simba B chini ya umri wa miaka 17. "Mimi sijawahi kusema nimeacha kucheza mpira na hata Simba hawajawahi kusema nimeacha bali waliniaga kwa heshima tu kuwa mchezaji wetu na ameitumikia timu yetu,. Hili linashangaza tu hapa kwetu ila mimi nimekuwa nikisoma ukocha toka muda na wakati nafundisha nilikuwa na majeraha na ile pia ilikuwa kama sehemu yangu ya field" John Bocco, alisema

Ni wakati sahihi wa Haji Manara kurudi Simba au kwenda Singida Black Stars

Picha
Na Prince Hoza MAISHA ya Haji Manara ndani ya klabu ya Yanga SC kwasasa si mazuri, na hiyo yote baada ya kumaliza adhabu yake aliyopewa na TFF, Manara alifungiwa mwaka 2022 kwa muda wa miaka miwili kwa kosa la kumshambulia kwa maneno makali Rais wa Shirikisho la soka nchini Wallace Karia. Yanga SC ilikosa huduma ya Afisa Habari wake kwa kosa hilo hivyo uongozi wa klabu hiyo uliamua kuajili mtu mwingine ili kuziba nafasi ya Manara, Ali Shabani Kamwe alichukua nafasi ya Manara na akawa Afisa Habari wa klabu hiyo kongwe na kubwa hapa nchini. Kamwe alikuwa mchambuzi wa Azam Tv, mwaka 2022 naye alianza kuhudumu kama bosi wa kitengo cha habari na moja kati ya sifa anazomiminiwa na mashabiki wa klabu hiyo ni kwamba ameliziba pengo la Manara vizuri. Wanayanga walifurahishwa sana na Alikamwe, na katika miaka miwili aliyohudumu akabeba nao mataji kiasi kwamba kuanzia mkurugenzi wa GSM ambao ni wawekezaji wa klabu hiyo na Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said kumkubali. Hata wakati Manara ameruhu...

Zuchu amzawadia gari Anjela

Picha
Msanii maarufu wa lebo ya WCB Zuchu amemzawadia gari aina ya Crown msanii mwenzake Anjela aliyekuwa lebo ya Konde Gang iliyochini ya Harmonize. Japo wengi walidhani ni mzaha na kiki, Msanii wa Bongofleva Zuchu ametimiza ahadi ya kumnunulia msanii mwenzake Anjela gari aina ya Crown

AFL KUFANYIKA MWAKANI AFRIKA KUSINI, SIMBA NA YANGA NDANI

Picha
Shirikisho la soka Afrika, CAF limetoa orodha ya vilabu (24) vitakavyoshiriki michuano ya African Football League itakayofanyika mwaka ujao nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 11 mpaka 9 Februari 2025. CECAFA ZONE (4) : Young Africans SC Simba SC Al-Hilal Omdurman Al-Merrikh COSAFA ZONE (4) Mamelodi Sundowns Orlando Pirates Petro Atletico de Luanda Marumo Gallants UNAF ZONE (8) : Al Ahly Cairo Wydad Casablanca RS Berkane Zamalek SC Raja Casablanca USM Alger CR Belouizdad Esperance Tunis UFOA & UNIFFAC ZONE (8) : TP Mazembe ASEC Mimosas Horoya AC Rivers United Cotton de Garoua FC Nouadhibou AS Vita Club Enyimba

Dabo ana presha ya kufukuzwa Azam FC

Picha
Kocha mkuu wa timu ya Azam FC Youssouph Dabo amesema yeye wala haofii kufutwa kazi kwani katika maisha yake ya soka haogopi kabisa. Dabo amesema kabla ya kufundisha Azam FC alikuwa anafanya kazi hiyo hiyo ya ukocha hivyo ataendelea kuwa kocha hata kama akifukuzwa kazi na waajiri wake. "Kabla ya Azam FC nilikuwa kocha na baada ya Azam FC pia nitaendelea kuwa kocha, hivyo sina presha ya kufukuzwa." Alisema Youssouph Dabo Kocha wa Azam FC.

JKT Tanzania yaibana mbavu Azam FC

Picha
Timu ya JKT Tanzania jioni ya leo imeilazimisha sare isiyo na magoli 0-0 Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara katika uwanja wa Meja Isamuya jijini Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC ambao wametokea nchini Rwanda walikocheza na APR michuano ya Ligu ya mabingwa Afrika na kutupwa nje kwa kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1

AL AHLI TRIPOLI YARUHUSIWA KUMTUMIA MABULULU, SIMBA KAZI WANAYO

Picha
Klabu ya Al-Ahli Tripoli imethibitisha kuwa wamepata kibali kutoka CAF cha kumtumia mshambuliaji wao mpya Mabululu, Mabululu alisajiliwa katika dirisha hili kubwa lililopita akitokea Al-Ittihad ya Egypt hakucheza mechi yoyote kwa sababu hakuwa na vibali, wameruhusiwa kumtumia kuanzia mechi zijazo za CAF. Takwimu zake za ligi kuu ya Egypt akiwa Al-Ittihad katika misimu 3 Season : 23/24 Magoli 11 (mfungaji wa sita) Assist 5 Season : 22/23 Magoli 16 Asist 1 Season : 21/22 Magoli 13 Assist 2

Mdaka mishale wa Simba aitwa timu ya taifa

Picha
Golikipa wa Simba SC Moussa Pinpin Camara (25) ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Guinea kitakachocheza mechi mbili za kufuzu AFCON 2025. Mchezo wao dhidi ya DR Congo na Tanzania, Camara anatajwa kuwa kipa namba mbili wa timu ya taifa

Aziz Andambwile amjibu Awesu Awesu

Picha
Baada ya mchezaji mpya wa timu ya Simba SC Awesu Awesu kuposti akiwa na gari lake alilonunua kutokana na fedha za usajili alizopewa na Simba, nyota mwenzake Aziz Andambwile amemjibu kwa kuposti picha yake akiwa na gari lake. Andambwile aliyesajiliwa na Yanga akitokea Singida Fountain Gate, ameposti picha akiwa kwenye gari lake ambalo amelipata baada ya kusajiliwa na Yanga Aziz Andambwile

Fadlu ataka vijana watano kupandishwa fasta timu ya wakubwa

Picha
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Fadlu Davids ametoa agizo la kupandishwa kwa wachezaji watano kutoka katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kwenda katika kikosi cha wakubwa ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi kwa wachezaji wawili, Daruwesh Ahmed na Okech Nyembe kutumika kwenye ligi. . Kocha huyo ameagiza kwamba wachezaji hao watano wawe wanashiriki kwa asilimia 100 katika programu za timu kwa maana ya kambi, mazoezi ya pamoja na kupata huduma zote ambazo wanapata wachezaji wa kikosi ha wakubwa.

UEFA kumpa tuzo maalum Cristiano Ronaldo

Picha
Cristiano Ronaldo atapokewa tuzo maalumu kutoka Chama cha soka Barani ulaya(UEFA) ya kuwa mchezaji bora wa muda wowote katika mashindano ya ligi ya mabingwa na kuwa mfungaji wa muda wowote wa mashindano ya ligi ya mabigwa barani ulaya. Tuzo hiyo atapewa siku ya Alhamisi ambapo itakuwa na sherehe za upangaji wa makundi ya ligi ya mabingwa ulaya yatayofanyika Monacco.

Msuva, Samatta watemwa Stars, Job arejeshwa

Picha
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea. Simon Msuva (30) na Mbwana Samatta (31) wote wamekosekana kwenye kikosi hicho. Dickson Job amerejeshwa kikosini.

Hatimaye Haji Manara awa Mtendaji mkuu wa hamasa Yanga Fans

Picha
Uongozi wa klab ya Yanga rasmi umembadilishia majukumu aliyekuwa msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara na kuwa Mtendaji mkuu wa Kitengo hamasa ndani ya Yanga FANS ENGAGEMENTS, Sasa Haji anaenda Kuongeza Nguvu ili kuisaidia Mabadiliko ndani ya klab ya Yanga kwenye zoezi la Usajili wa wanachama na mashabiki wa Yanga.

Simba kujifua na Al Hilal

Picha
Agosti 31, Simba SC watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal . Kocha Fadlu amehitaji mchezo wa kirafiki wa kujipima kabla ya kuvaana na Al Ahli Tripoli kwenye CAFCC.

Awesu Awesu akiwa na ndinga lake

Picha
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC Awesu Ally Awesu ameposti akiwa na ndinga lake (crown) alilonunua baada ya kusajiliwa na Wekundu hao wa Msimbazi. Baadhi ya watu wanasema kwamba gari aliloposti Awesu alinunuliwa na Rais wa Yanga, Injinia Hersi, ingawa hakuna uhakika kama ni kweli. Mambo Uwanjani Blog inafahamu kwamba Awesu amevuna mpunga wa maana Simba SC

Kocha wa Mtibwa Sugar ashangaza kwa kutumia fimbo

Picha
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Melis Medo amekuwa akitumia fimbo katika Uwanja wao wa mazoezi Manungu Complex, Morogoro. Mtibwa Sugar inayoshiriki Championship msimu huu imekuwa na mwalimu huyo ambaye anapenda kutumia fimbo katika ufundishaji wake. Kocha huyo raia wa Marekani alivyokuwa anakinoa kikosi cha Coastal Union ya Tanga alikuwa akitumia fimbo hiyo katika Viwanja vya Popatraly.

Waarabu wa Simba Al Ahli Tripoli hawa hapa

Picha
Na Ayoub Taarifa MAJINA KAMILI ; Wanaitwa AL AHLI SC TRIPOLI kutoka Nchini Libya na wanafahamika pia kwa jina la utani la Bianco Verde (Timu ya Karne) Timu hii ilianzishwa Septemba 19 1950, Klabu namba mbili yenye mafanikio zaidi katika soka la Nchi ya Libya 🏆 ×13 Libya Premier league 🏆 ×7 Libyan Cup 🏆 ×2 Libyan Super Cups Wamepata nafasi ya kucheza Kombe la shirikisho msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Al Nassr na Al Hilal za Libya MAFANIKIO YAO MAKUBWA ZAIDI AFRIKA Al Ahli Tripoli wamecheza Robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mara moja & Mwaka 2022 walicheza Nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika wakatolewa na Orlando Pirates ambao walimuondoa Simba SC kwa Matuta 1st Leg | Al Ahli Tripoli 0-2 Orlando Pirates 2nd Leg| Orlando Pirates 0-1 Al Ahli Tripoli WACHEZAJI WAO GHALI ZAIDI Staa wa Angola, Straika wa Magoli Agustinō Cristovao Pacienćia "MABULULU" (32) ndiye mchezaji Ghali zaidi katika kikosi hicho akisajiliwa katika diri...

Boka, Baleke ruksa kuivaa CBE

Picha
Wachezaji, Chadrack Boka na Jean Baleke baada ya kukosa michezo ya awali CAF Champions League sasa wako huru kucheza hatua inayofuata CAF champions League. ITC za Chadrack Boka na Baleke zilichelewa kufika, zilifika wakati ambao dirisha la CAF likiwa limefungwa.

Bodi ya Ligi yapangua ratiba Ligi Kuu bara

Picha
Bodi ya Ligi (TPLB) imepangus ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa timu za Yanga, Simba na Azam na sasa imeweka mkeka mpya unaozihusu timu hizo kwenye ligi hiyo. Mechi ya Simba na Yanga iko pale oale Oktoba 19 lakini mechi nyingine zimebadilika tofauti na ratiba ya mwanzo ilivyosema. Na hii ndio ratiba kamili ikianza mabingwa watetezi Yanga na kufuatiwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC. Young Africans SC : ◉ Kagera vs Yanga - Aug 29 ◉ Yanga vs Mashujaa - Sep 14 ◉ Black Stars vs Yanga - Sep 20 ◉ Ken gold vs Yanga - Sep 25 ◉ Yanga vs KMC - Sep 29 ◉ Yanga vs Pamba - Oct 3 ◉ Simba vs Yanga - Oct 19 Simba Sports Club : ◉ Simba 3 - 0 Tabora - Aug 18 ◉ Simba 4 - 0 Fountain Gate - Aug 25 ◉ Azam vs Simba - Sept 14 ◉ Simba vs Namungo - Sep 20 ◉ Dodoma Jiji vs Simba - Sep 29 ◉ Simba vs Coastal - Oct 4 ◉ Simba vs Yanga - Oct 19 Azam Football club : ◉ JKT vs Azam - Aug 28 ◉ Azam vs Simba - Sept 14 ◉ Azam vs Coastal - Sep 20 ◉ KMC  vs  Azam - Sep 26 ◉ Mashujaa  vs  ...

JB akiri Mariam ni staa wa kike bongomuvie

Picha
"Naomba nikiri leo kuwa Mariam Ismail ni mmoja kati ya waigizaji watatu wa kike ambao wakiwa set naduwaa kuwaangalia na nikipangwa nao najiandaa kwa muda mrefu. Hajawahi kupata tuzo masikini wala hana followers wengi, lakini kwangu ni mmoja wa waigizaji bora tulionao" ~JB, Muigizaji filamu Bongo. "Mungu akupe afya njema uzidi kutupa raha, jamani sio Birthday yake, nimejisikia tu kumpa maua yake na nitakuwa na utaratibu huu wa kuwapa maua na wengine " ~JB.