Dabo ana presha ya kufukuzwa Azam FC
Kocha mkuu wa timu ya Azam FC Youssouph Dabo amesema yeye wala haofii kufutwa kazi kwani katika maisha yake ya soka haogopi kabisa.
Dabo amesema kabla ya kufundisha Azam FC alikuwa anafanya kazi hiyo hiyo ya ukocha hivyo ataendelea kuwa kocha hata kama akifukuzwa kazi na waajiri wake.
"Kabla ya Azam FC nilikuwa kocha na baada ya Azam FC pia nitaendelea kuwa kocha, hivyo sina presha ya kufukuzwa."
Alisema Youssouph Dabo Kocha wa Azam FC.