Sijawahi kusema nimestaafu soka- Bocco
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, John Raphael Bocco ameshangazwa na taarifa kwamba yeye alitangaza kustaafu soka.
Bocco amesema yeye hajaacha soka na ataendelea kucheza mpaka pale atapoacha mwenyewe, Bocco alionekana akisomea ukocha na ilielezwa kwamba amestaafu soka na atakuwa kocha wa timu ya Simba B chini ya umri wa miaka 17.
"Mimi sijawahi kusema nimeacha kucheza mpira na hata Simba hawajawahi kusema nimeacha bali waliniaga kwa heshima tu kuwa mchezaji wetu na ameitumikia timu yetu,.
Hili linashangaza tu hapa kwetu ila mimi nimekuwa nikisoma ukocha toka muda na wakati nafundisha nilikuwa na majeraha na ile pia ilikuwa kama sehemu yangu ya field" John Bocco, alisema