Simba, Al Hilal hakuna mbabe
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika uwanja wa KMC Complex Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Simba walitangulia kupata kupitia kwa mshambuliaji mpya aliyetambulishwa kwenye mchezo huo Lionel Atebe dakika ya 26, kabla ya Al Hilal inayonolewa na Ibenge raia ya DR Congo dakika ya 76 kupitia kwa Serge Pokou.
Hata hivyo Suleiman Ezala wa Al Hilal dakika ya 55 alioneshwa kadi nyekundu na kushindwa kuendelea na mchezo, Simba itaendelea kushuka tena ueanjani kucheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa