Kocha wa Mtibwa Sugar ashangaza kwa kutumia fimbo
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Melis Medo amekuwa akitumia fimbo katika Uwanja wao wa mazoezi Manungu Complex, Morogoro.
Mtibwa Sugar inayoshiriki Championship msimu huu imekuwa na mwalimu huyo ambaye anapenda kutumia fimbo katika ufundishaji wake.
Kocha huyo raia wa Marekani alivyokuwa anakinoa kikosi cha Coastal Union ya Tanga alikuwa akitumia fimbo hiyo katika Viwanja vya Popatraly.