JKT Tanzania yaibana mbavu Azam FC
Timu ya JKT Tanzania jioni ya leo imeilazimisha sare isiyo na magoli 0-0 Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara katika uwanja wa Meja Isamuya jijini Dar es Salaam.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC ambao wametokea nchini Rwanda walikocheza na APR michuano ya Ligu ya mabingwa Afrika na kutupwa nje kwa kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1