Fadlu ataka vijana watano kupandishwa fasta timu ya wakubwa
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Fadlu Davids ametoa agizo la kupandishwa kwa wachezaji watano kutoka katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kwenda katika kikosi cha wakubwa ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi kwa wachezaji wawili, Daruwesh Ahmed na Okech Nyembe kutumika kwenye ligi.
.
Kocha huyo ameagiza kwamba wachezaji hao watano wawe wanashiriki kwa asilimia 100 katika programu za timu kwa maana ya kambi, mazoezi ya pamoja na kupata huduma zote ambazo wanapata wachezaji wa kikosi ha wakubwa.