Yanga yaiduwaza Kagera Sugar nyumbani kwao
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga SC imeilaza Kagera Sugar mabao 2-0 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Huo ndio wa kwanza kwa Yangs hivyo wamefikisha pointi tatu wakati Kagera Sugar wamecheza mechi ya pili huku zote wakifungwa.
Maxi Nzengeli dakika ya 26 alitangulia kufunga bao la kuongoza kwa mabingwa hao kabla ya Clement Mzize dakika ya 88 kufunga bao la pili na kuhitimisha ushindi wa mabao mawili.
Wakati huo KMC FC ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex, Kinondoni, Ibrahim Elas alianza kufunga kwa upande wa KMC kabla ya Maabad Maulid kusawazisha kwa mkwaju wa penalti