Baba yake Samatta awalilia Msuva na mwanae Taifa Stars
"Inaonekana kuna aina fulani ya chuki kutokana na mafanikio ya mwanangu Mbwana, bado Mbwana ana nafasi kubwa sana katika timu ya taifa, Samatta na Msuva ni wachezaji muhimu sana kwenye taifa letu, kwa asilimia kubwa wao ndio wamesababisha tufuzu kucheza AFCON zote mbili
"Kwenye kombe la dunia 1966, Pele alipata majeraha dhidi ya Ureno lakini mechi iliyofuata alicheza kwa sababu alipigwa sindano ya ganzi na wakawa wanamuogopa sababu yupo nje; hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa Samatta vivyo hivyo kwa Msuva
Kocha Hemed Morocco amekosea sana kuwaacha Samatta na Simon Msuva, Mzee Ally Samatta Baba mzazi wa Mbwana Samatta