JKT Tanzania haiwezi kugambania ubingwa na Yanga au Simba- Jemedari

Na Salum Fikiri Jr

CEO wa JKT Tanzania, Jemedari Said Kazumali amedai kwamba timu yake haitaweza kugombania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara wala kufika tatu bora, isipokuwa nafasi ambayo wanaweza kushindana nayo ni ya kutoshuka daraja.

Jemedari ambaye pia ni mchambuzi wa kwenye redio Crown FM inayomilikiwa na mwanamuziki Alikiba, ameshangaa kauli ikitolewa na Afisa Habari wa klabu ya JKT Tanzania Masau Bwire kwamba msimu huu wanataka kugombania ubingwa na Yanga pamoja na Simba.

Jemedari amedai kwamba kushindania ubingwa na Yanga au Simba si jambo rahisi kama watu wanavyodhani, timu yake ya JKT Tanzania nafasi ambayo wanaweza kuishindania ni ya kutoshuka daraja kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo waliangukia play off


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA