Haji Mnoga akamilisha usajili Salford City
Beki wa kimataifa wa Tanzania, Haji Mnoga amekamilisha usajili wake kuelekea katika Klabu ya Salford City, iliyopo Jiji la Manchester Nchini Uingereza.
Mnoga amesaini mkataba wa mwaka mmoja (mpaka 2025) na Klabu hiyo akitokea katika Klabu ya Portsmouth kama mchezaji huru.
Salford City ni Klabu inayoshiriki Ligi daraja la pili Kiwango cha nne kwenye wa mfumo wa Ligi Nchini Uingereza.
Hivi sasa iko katika nafasi ya 20 kwenye msimamo wa Ligi hiyo yenye timu 24 katika michezo mitatu.