Godbless Lema aziombea mabaya Simba na Yanga
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Godbless Lema amewashangaa Watanzania kuendelea na msingi wa mawazo kwamba Simba na Yanga zina maana sana kuliko kujali maisha ya watu.
Lema amedai kwamba kama angekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu ili aziue kabisa timu hizo kwani zinachelewesha maisha ya Watanzania.
Mwanasiass huyo aliyerejea nchini baada ya kuwa uhamishoni wakati wa utawala wa Awamu ya tano chini ya Dkt John Magufuli, anadai maisha ya Watanzania yanahitaji fikra pana, lakini Simba na Yanga zinaharibu mipango kwani kila mtu anawaza Simba na Yanga.
"Watanzania mkiendelea na huu msingi wa mawazo mliyonayo ya kwamba Mpira wa Simba na Yanga unamaana kuliko maisha ya wenzenu, hii nchi ni ya ajabu.
Mimi ningekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu aziue SIMBA na YANGA zisiwepo nchi hii ningeshukuru sana''
Alisema Godbless Lema