Pyramids mabingwa wa Misri, Mayele ahusika
Mshambuliaji Fiston Mayele raia wa DR Congo, amekuwa na msimu mzuri baada ya kuisaidia timu yake ya Pyramids ya Misri kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Mayele amrhusika kwa asilimia 100 timu hiyo kushinda ubingwa huu kwani yeye ndiye chachu kubwa ya timu kuhahakisha inapata ushindi wastani kwa kila mechi.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga SC ya Tanzania ambayo nayo aliipa ubingwa misimu miwili mfululizo, mpaka msimu unamalizika, Mayele aliibuka mfungaji bora wa klabu hiyo.
Mayele amefunga magoli 17 ambapo pia ameweza kuwa mfungaji bora namba mbili wa ligi ya nchi hiyo