Diamond, Alikiba na Harmonize kuwania tuzo za mwanamuziki bora Tanzania

Kamati ya Tanzania Music Award (TMA) leo August 29,2024 imeanza kutangaza Nominees wanaowania tuzo za muziki Nchini kwa kuanza na category tatu ambazo ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Wimbo bora wa taarabu wa mwaka kuna Watu na Viatu ya Malkia Layla Rashid, Hatuachani ya Amina Kidevu, Bila Yeye Sijiwezi ya Mwinyi Mkuu, Sina Wema ya Mwasiti Mbwana na DSM Sweetheart ya Salha.

Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna People ya Libianca, American Love ya Qing Madi, Lonely at the Top ya Asake, Unavailable ya Davido ft Musa Keys na Mnike ya Tyler ICU.

Kwa upande wa Mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume kuna Marioo kupitia wimbo wa Shisha , Diamond Platnumz kupitia Shuu, Harmonize kupitia Single Again , Alikiba kupitia Sumu na Jay Melody kupitia wimbo wa Nitasema

Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema category nyingine zitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifumgulowa rasmi September 3


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA