Simba Queens yaangukia nafasi ya nne CECAFA
Timu ya Simba Queens imeambulia nafasi ya nne katika mashindano ya CECAFA Winners Cup kwa wanawake baada ya kufungwa mabao 2-0 na timu ya Kawempe Muslim.
Mabingwa hao wa ligi ya wanawake Tanzania, imeshundwa kushangaza kwa kutupwa mapema kwenye michuano hiyo ambapo bingwa wake anakwenda kushiriki Ligi ya mabingwa Afrika.
Msimu juzi Simba Queens ilienda kushiriki michuano hiyo ya Afrika na ilifika hadi nafasi ya nne, kushindwa kwa mwaka huu kumezua sintofahamu nyingi kwa wapenzi wa soka la wanawake na isitoshe timu imeandaliwa vizuri