Waarabu wa Simba Al Ahli Tripoli hawa hapa
Na Ayoub Taarifa
MAJINA KAMILI ; Wanaitwa AL AHLI SC TRIPOLI kutoka Nchini Libya na wanafahamika pia kwa jina la utani la Bianco Verde (Timu ya Karne)
Timu hii ilianzishwa Septemba 19 1950, Klabu namba mbili yenye mafanikio zaidi katika soka la Nchi ya Libya
🏆 ×13 Libya Premier league
🏆 ×7 Libyan Cup
🏆 ×2 Libyan Super Cups
Wamepata nafasi ya kucheza Kombe la shirikisho msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Al Nassr na Al Hilal za Libya
MAFANIKIO YAO MAKUBWA ZAIDI AFRIKA
Al Ahli Tripoli wamecheza Robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mara moja & Mwaka 2022 walicheza Nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika wakatolewa na Orlando Pirates ambao walimuondoa Simba SC kwa Matuta
1st Leg | Al Ahli Tripoli 0-2 Orlando Pirates
2nd Leg| Orlando Pirates 0-1 Al Ahli Tripoli
WACHEZAJI WAO GHALI ZAIDI
Staa wa Angola, Straika wa Magoli Agustinō Cristovao Pacienćia "MABULULU" (32) ndiye mchezaji Ghali zaidi katika kikosi hicho akisajiliwa katika dirisha hili kwa Bil 2 za Kitanzania
Mchezaji mwingine ghali zaidi katika Kikosi chao ni Winga Hamdoi El Houni (30) aliesajiliwa kutoka Wydad Casablanca kwa uhamisho wa bure ana thamani ya Mil 800+ za Kitanzania
KOCHA MKUU
Kocha mkuu wa Klabu hii ni Chokri Khatoi raia wa Tunisia ambae amewahi kupita Abu Salim ya Libya na Stade Tunisien ya Tunisia
TOP SCORER : Ahmed Mohammed Rajab Krawas (35) ndiye nyota aliefunga mabao mengi zaidi katika msimu uliomalizika (12)
Al Ahli Tripoli anatumia Uwanja wa Libya Tripoli International kama uwanja wao wa nyumbani wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 45,000 waliokaa
Wanatumia jezi za kijani katika mechi zao za nyumbani na wanatumia rangi Nyeupe wakiwa Ugenini
▪️THAMANI YAO : Kwa mujibu wa Transfer Market thamani ya Kikosi cha Al Ahli Tripoli ni Bil 6 za Kitanzania
▪️Mara ya mwisho kwa Al Ahli Tripoli kucheza katika Ardhi ya TANZANIA ilikua ni mwaka 2021 wakipoteza 2-0 kwa Biashara United MARA