Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Bodi ya Ligi yapangua ratiba Ligi Kuu bara

Bodi ya Ligi (TPLB) imepangus ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa timu za Yanga, Simba na Azam na sasa imeweka mkeka mpya unaozihusu timu hizo kwenye ligi hiyo.

Mechi ya Simba na Yanga iko pale oale Oktoba 19 lakini mechi nyingine zimebadilika tofauti na ratiba ya mwanzo ilivyosema.

Na hii ndio ratiba kamili ikianza mabingwa watetezi Yanga na kufuatiwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Young Africans SC :

◉ Kagera vs Yanga - Aug 29
◉ Yanga vs Mashujaa - Sep 14
◉ Black Stars vs Yanga - Sep 20
◉ Ken gold vs Yanga - Sep 25
◉ Yanga vs KMC - Sep 29
◉ Yanga vs Pamba - Oct 3
◉ Simba vs Yanga - Oct 19

Simba Sports Club :

◉ Simba 3 - 0 Tabora - Aug 18
◉ Simba 4 - 0 Fountain Gate - Aug 25
◉ Azam vs Simba - Sept 14
◉ Simba vs Namungo - Sep 20
◉ Dodoma Jiji vs Simba - Sep 29
◉ Simba vs Coastal - Oct 4
◉ Simba vs Yanga - Oct 19

Azam Football club :

◉ JKT vs Azam - Aug 28
◉ Azam vs Simba - Sept 14
◉ Azam vs Coastal - Sep 20
◉ KMC  vs  Azam - Sep 26
◉ Mashujaa  vs  Azam - Sep 29
◉ Namungo  vs  Azam - Oct 3

◉ Prisons  vs  Azam - Oct 18

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa